Marianna Bergues, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anaishi mjini Narbeth, Pennsylvania. Nyakati zote amependa kuandika. Alipokuwa na umri wa miaka saba, babake alimsimulia hadithi ya rafikiye mjini Paris aliyejitolea kuwatunza wanyama vipenzi wa marafiki zake. Mamake (Roseland Bergues) alimtia moyo wa kuandika rasimu ya hadithi hiyo. Hadithi hio iliandikwa, ikahifadhiwa, na kusahaulika. Mwaka wa 2014, hadithi hiyo iliyopatikana ilimvutia Marianna na ubunifu wake tena. Mamake na babake wakamtia moyo wa kukamilisha hadithi hiyo na kuishiriki na wengine. Kwa hadithi hiyo, anamshukuru babake, Christian Bergues, aliyezaliwa na kulelewa nchini Ufaransa. Ni kwa ajili yake kitabu hiki kipo. Ilikuwa msukumo wake na usaidizi wake katika uandishi uliofanya kitabu hiki kuwezekana.